0

UNAWEZA KUJIUNGA NASI HAPA MOJA KWA MOJA ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..

Na Jane Charles, Kahama.
26/11/2016.
Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga imewataka wananchi waishio mjini, kutolima mazao katika maeneo yao bila kupewa kibali kutoka halmashauri hiyo kinachoelekeza namna ya kuzingatia sheria ya ardhi.


Akizungumza na Blogu hii, Kaimu afisa kilimo wa halmashauri hiyo, Fidei Sumuni, amesema zipo sheria zinazoelekeza shughuli za kilimo katika maeneo ya Mjini.

Amesema sheria ya kilimo cha Mjini namba 242 ya mwaka 2008 kanuni ya 13 imeleeza wakulima kupata kibali cha kuendesha shughuli zozote katika maeneo yao, hivyo ni kosa kulima mazao mjini.
Aidha pamoja na mambo mengine sheria hiyo imeelekeza mazao yanayopaswa kulimwa ni yale yasiyozidi urefu wa futi tatu.

Katika hatua nyingine, Sumuni amewashauri wakulima kulima mazao ya muda mfupi na yanayostahimili ukame kutokana na mabadliko ya hali ya hewa yaliyotangazwa na Mamlaka ya hali ya Hewa nchini, TMA.
www.ndalike.blogspot.com

LIKE PAGE YETU HAPA CHINI

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Facebook Plugin by NDALIKE SONDA MEDIA

Post a Comment

 
Top