0

UNAWEZA KUJIUNGA NASI HAPA MOJA KWA MOJA ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..

Na,Michael Francis, Kahama.
26/11/2016.
   Baadhi ya wakulima katika kijiji cha Wendele Wilayani Kahama  Mkoani Shinyanga Wameiomba serikali kuwasaidia kuwatafutia  mbegu zinazostahimili ukame ili kukabiliana na Baa la njaa.

Kauli hiyo imetolewa na Wakulima hao  kufuatia taarifa iliyotangazwa na mamlaka ya hali ya hewa  nchini TMA, mapema mwanzoni mwa msimu wa kilimo ambapo mamlaka hiyo ilitoa taarifa kuwa msimu huu wa kilimo kutakuwa na mvua za wastani hivyo wakulima wachukue tahadhari ya kulima mazao yanayostahimili ukame.

Wakulima hao wamesema   serikali haina budi kuwaletea mbegu hizo ikiwemo     mbegu za mtama, na mihogo ili waweze kuzitumia na kukabiliana na hali itakayokuwepo mwaka huu ya mvua za wastani.

Diwani wa kata hiyo ya wendele Kilunga Justine amesema Wananchi wenyewe wanatakiwa kutambua kuwa suala la kutafuta mbegu zinazostahimili ukame siyo la serikali pekee na kuwahimiza kufanya juhudi zao wenyewe za kupata mbegu hizo.

Zaidi ya kaya 1000  zilizopo katika kijiji cha wendele zina hitaji mbegu hizo zinazostahimili ukame ili kukabiliana na hali ya uwepo wa mvua za wastani iliyotangazwa mwaka huu na mamlaka ya hali ya hewa.
www.ndalike.blogspot.com

LIKE PAGE YETU HAPA CHINI

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Facebook Plugin by NDALIKE SONDA MEDIA

Post a Comment

 
Top