UNAWEZA KUJIUNGA NASI HAPA MOJA KWA MOJA ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Hatimaye Masomo kwa ajili ya
wanafunzi wa shule ya msingi Mwakata wilayani Kahama, Shinyanga yananza
jumatatu baada ya kukatishwa kwa zaidi ya siku 10, kutokana na madasa ya shule
hiyo kutumika kuhifadhi misaada na
wananchi waliokuwa wamekubwa na maafa ya
mvua ya mawe yaliyotokea machi 3 mwaka huu katika kata hiyo.
Akizungumza na Nipashe
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Idd Ginila alisema masomo yameanza rasmi jumatatu
ambapo zoezi la awali lilikuwa ni kuwagawia wanafunzi vifaa vya shule ambavyo ni sehemu ya msaada
vilivyotolewa na wananchi, makampuni na taasisi mbalimbali.
Alisema walitumia misikiti,
makanisa pamoja na uongozi wa serikali
ya kijiji kuwatangazia wazazi na walezi kuwahimiza wanafunzi, kuhudhuria masomo
yao.
“Tulitangaza kuanzia ijumaa
kule msikitini, pia tulifanya hivyo siku ya jumamosi na jumapili kutangaza
makanisani, na jumatatu tumegawa vitu
vyote vya misaada ambavyo ni madaftari, karamu, penseli na vifaa vingine kwa
wanafunzi.”alisema Mwalimu mkuu.
Katika hatua nyingine Mkuu
huyo wa shule alisema changamoto iliyopo ni ukosefu wa matundu manne ya choo
cha wavulana kutokana na kile cha awali kubomolewa na mvua na kwamba kwa sasa
wanatumia vyoo vya muda vilivyokuwa vikitumika wakati wa kambi huku uchimbaji
wa matundu mengine ukuendelea na utakamilika bada ya siku 14.
Kwa uapande wake mkuu wa wilaya ya Kahama Benson
Mpesya alisema tayari watu waliokuwa katika kambi ya shule ya msingi Mwakata
wamekwisha kuhamia katika nyumba zao za muda zilizojengwa na serikali huku
baadhi ya watu ambao nyumba zao hazijakamilika wakihamishiwa katika jingo la
chuo cha walemavu lililopo kijijini hapo.
Alisaema kufuatia kukatishwa kwa masomo kwa zaidi ya siku kumi,
tayari wameshafanya mpango wa kufidishia siku hizo ambapo wakati wa rikizo fupi
wataendelea ka muda wa wiki moja na tayari walimu wamekwishwa kufahamishwa.
LIKE PAGE YETU HAPA CHINI
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by NDALIKE SONDA MEDIA
Post a Comment