UNAWEZA KUJIUNGA NASI HAPA MOJA KWA MOJA ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
![](https://scontent-mxp1-1.xx.fbcdn.net/v/t1.0-9/14938391_1087000468089109_6637985371247186549_n.jpg?oh=05013d7bf37880f279d75c733ed508a5&oe=58BFBDEF)
MGOMBEA WA NAFASI YA MWEKA HAZINA WA CHAMA CHA SOKA WILAYA YA KAHAMA KDFA, NDALIKE SONDA.
Tayari Mchakato wa Kampeni ulianza tangu Novemba 8 mwaka huu, na utakamilika Novemba 14 mwaka huu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi siku ya jumannne ijayo 15/11/2016.
Akizungumza na Blogu hii, Sonda ambaye kitaaluma ni Mwandishi mahari wa Habari, alisema ameama kuchukua nafasi hiyo kwa kuwa anaieza na anauwezo wa kubuni vyanzo vingi vya mapato amabvyo vitakuwa msaada mkubwa kwa vilabu na chama cha soka.
"Ni kweli nimeanza kampeni zangu baada ya kamati ya Uchaguzi ya KDFA, Kuruhusu takribani siku tatu zimeppita sasa, Ila mimi malengo yangu ni kuhakikisha soka la Kahama linasonga mbele zaidi na njia pekeee ni kuimarisha mapato yatokanavyo na mpira wa miguu, na mtu pekee kati ya walioomba nafasi hiyo mwenye uwezo wa kusimamia hayo ni Mimi Ndalike Sonda" alisema Sonda. Nakuongeza.
"Hakuna asiyejua kuwa uongozi wa Chama cha soka hauna malipo na ndio maana inahitajika kupata viongozi wenye uwezo wa kujituma na wenye machungu zaid na soka la Kahama kuliko kutanguliza maslahi yao binafsi, Hakika wajumbe wote kutoka vilabu 24 wananchama wa KDFA Pamoja na FRAT Kahama hakikisheni mnanipa KURA zenu ili niwatumikie." Alionheza Sonda.
Aidha aliomba wapiga kura kuchagua viongozi wenye uwezo wa kiutendaji, katika nafasi zote ili kuwa na vviongozi wenye uwezoo wa kuchapa kazi.
Uchaguzi wa Chama cha soka utafanyika Jumanne ijayo novemba 15 mwaka huu, katika ukumbi wa Chuo cha uuguzi na ukunga mjini kahama.
www.ndalike.blogspot.com
LIKE PAGE YETU HAPA CHINI
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by NDALIKE SONDA MEDIA
Post a Comment