UNAWEZA KUJIUNGA NASI HAPA MOJA KWA MOJA ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
26/11/2016.
Jamii wilayani Kahama imetakiwa kuhakikisha inatoa ushirikiano kwa vyombo vinavyosimamia suala la ukatili wa kijinsia, kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati, ili kuwafichua wanaojihusisha na jambo hilo,
Hali hiyo itasaidia kukomesha vitendo vya ukatiri wilayani humo.
Kauli hiyo imetolewa jana, ijumaa na katibu wa tume ya utumishi wa walimu wilayani Kahama, TSC, Bashemela Seif, kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa kahama, Anderson Msumba, katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia nchini.
Seif amesema ni vyema jamii ikashirikiana na vyombo husika ili kukomesha vitendo hivyo ambapo amesema mpaka sasa matukio mbalimbali yanayohusisha kesi za ukatiLI wa kijinsia na watoto yametolewa taarifa kwa jeshi la Polisi na usatawi wa jamii.
Amesema matukio yanayoongoza tutotewa taarifa serikalini ni matukio ya kutelekeza watoto, kutupwa, ajira za utotoni , ukatili wa kimwili, mimba za utotoni, kubakwa, na kupigwa.
insert bashemela.
Akisoma risala mbele ya mgeni rasimi asikari kutoka Jeshi la Polisi, kitengo cha dawati la jinsia na watoto, Debora kizanga amesema licha ya elimu kutolewa kwa wananchi bado wananachi wamekuwa wakishindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi jambo amabalo linasababisha kukosa haki.
Maadhimisho ya siku 16 ya kupinga ukatiri wa kinjisia hufanyika kila mwaka kuanzia novemba 25 hadi disemba 10, na katika mji wa Kahama maadhimisho hayo yamezinduliwa katika ukumbi wa bwalo la polisi huku kauli mbiu ya mwaka huu ni “funguka pinga ukatili wa kijinsia”.
www.ndalike.blogspot.com
LIKE PAGE YETU HAPA CHINI
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by NDALIKE SONDA MEDIA
Post a Comment