UNAWEZA KUJIUNGA NASI HAPA MOJA KWA MOJA ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
09/12/2016.
Wananchi wa halmashauri ya Msalala wilayani Kahama wametakiwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali za kuboresha huduma za afya ili kuongeza ustawi wa jamii katika halmashauri hiyo.
Hayo yalisemwa leo na Kaimu Mganga mkuu wa halmashauri ya Msalala Dokta Ignas Lufulila wakati akizungumza na Baloha fm.
Dokta Lufulila aliwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika kusaidia kupatikana huduma za afya katika jamii.
Alisema, jukumu la kuboresha Huduna za afya kwa jamii siyo la serikali pekee, na hivyo wajitokeze kuchangia ujenzi wa miundombinu ya afya, pamoja na kutunza na kuilinda miundombinu hiyo.
Aidha Lufulila alitoa wito kwa wananchi kujiunga katika mfuko wa afya ya jamii CHF kwani mfuko huo ni moja kati ya mikakati ya serikali katika kuboresha huduma za Afya.
www.ndalike.blogspot.com
LIKE PAGE YETU HAPA CHINI
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by NDALIKE SONDA MEDIA
Post a Comment