UNAWEZA KUJIUNGA NASI HAPA MOJA KWA MOJA ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Timu ya soka ya Ambasador sc
ya mjini Kahama ambayo inashiriki ligi DARAJA LA PILI NGAZI YA Mkoa wa
Shinyanga pamoja na Kagongwa United yenye masikani yake katika mji mdogo wa
Kagongwa zitacheza mechi ya kirafiki juma pili hii machi 15 mwaka huu.
Mchezo huo ambao utapigwa
katika uwanja wa shule ya Msingi Kagongwa ni MAALUM kwa ajili ya kupata fedha
ambazo zitawasilishwa kwa waathirika wa
Mvua yam awe iliyoambatana na upepo mkali katika kata ya Mwakata ambapo mchango
huo utawasilishwa kupitia kamati ya maafa ya wilaya ya Kahama ambayo imeweka
kambi katika kata ya Mwakata.
Tayari maandalizi ya mchezo
huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kufanya matangazo katika vijiji vyote
vinavyozunguka kata ya kagongwa pamoja
na kupanga utarabu wa viingilio katika mchezo huo ambapo kiingilio kitakuwa ni
shilingi 500 kwa kila mshabiki atakayeingia.
Afisa habari wa Klabu ya
Ambasador Ndalike Said Sonda “Kocha Mkongwe” aliwataka mashabiki kujitokeza kwa
wingi kyazama mchezo huo ili kupata
fedha nyingi ambazo zitawasilishwa mapema wiki ijao kwa wahusika wa maafa hao.
Aidha alisema, mbali na
kiingilio hicho pia wadau wanaruhusiwa kuja na vitu vingine kama mchele Unga mabati Mbao kuku n.k ambavyo vitakusanywa
tayari kupelekwa katika kijiji cha
Mwakata kwa walengwa.
Sonda alisema mchezo huo pia utahidhiriwa na viongozi
mbalimbali wa chama cha soka wilaya ya Kahama KDFA, Viongozi wa Serikali, Dini
na hata Siasa hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi kwamni mabli na kuchangia
maafa pia timu hizo ni Mahasimu wa kubwa
wa soka hapa wilayani Kahama.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Kagongwa United Dogo Mshashi aliiambia blogu hii kwamba wadau wa soka wanapaswa kukuswa kutokana na
mchezo huo ni njia ya kuwakumbuka waathirika
wa maafa hayo pamoja na wale waliopoteza Maisha.
LIKE PAGE YETU HAPA CHINI
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by NDALIKE SONDA MEDIA
Post a Comment