UNAWEZA KUJIUNGA NASI HAPA MOJA KWA MOJA ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Imeelezwa kuwa nusu ya
wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Mwakata Wilayani Kahama Mkoani
Shinyanga wameshindwa kuhudhuria masomo
yao kutokana na wengi wao kuwa hana sare za shule kutokana na kuharibiwa na
mvua ya mawe iliyonyesha machi 3 mwaka huu.
Wanafunzi hao wameshindwa
kufika shuleni licha ya jamii kutangaziwa kuwahimiza wanafunzi wahudhuria
masomo baada ya kusitishwa kwa muda kutokana na kutokea kwa maafa
yaliyosababishwa na mvua ya mawe.
Akizungumza na Nipashe ofisini
kwake Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mwakata, Iddi Ginila alisema shule hiyo
ina jumla ya wanafunzi 736 ambapo waliohudhuria masomo kuanzia jumatatu
na jumanne ni zaidi ya 340, huku
wanafunzi 53 wakihudhuria masomo bila sare za shule.
Alisema wanafunzi ambao
hawajahudhuria masomo sababu kubwa imetajwa kuwa hawana sare za shule kutokana na makazi yao
kusombwa na maji, huku wengine wakiwa familia zao zikihangaikia makazi.
Hata hivyo alisema tayari
wamefanya ugawaji wa madaftari kwa wanafunzi waliohudhuria ambapo kila mwanafunzi
amepewa Madaftari 9 na zilizobaki zitatolewa kwa wanafunzi ambao bado
hawajahudhuria masomo.
Marrynasi Rafael ambaye ni
mwalimu wa shule hiyo alipongeza juhudi za serikali kwa kurejesha masomo kwani
changamoto kubwa ilikuwa ni kwa wanafunzi wa darasa la nne na darasa la saba
ambao wanakabiliwa na mitihani ya taifa.
Nao baadhi ya wanafunzi
waliozungumza na Nipashe wamefurahia kuanza kwa masomo huku wakiwataka
wanafunzi wenzao kufika shuleni kuendelea
na masomo.
LIKE PAGE YETU HAPA CHINI
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by NDALIKE SONDA MEDIA
Post a Comment