UNAWEZA KUJIUNGA NASI HAPA MOJA KWA MOJA ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
RAIS John Magufuli ambaye tangu Novemba 17, mwaka huu alikuwa katika
Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma kwa majukumu mbalimbali, amerejea Dar es
Salaam jana na wakati wowote inaelezwa kwamba anaweza kutangaza Baraza
la Mawaziri linalosubiriwa kwa hamu na Watanzania.
Dk Magufuli alitua Ikulu ya Chamwino, Novemba 17 kwa kutumia usafiri wa
barabara akisafiri kwa zaidi ya kilometa 300 kwenda katika Makao Makuu
ya Serikali ambako kwanza alikuwa na majukumu mawili makubwa.
Dk Magufuli alirejea Dar es Salaam huku tetesi zikiimarika kwamba
atatangaza baraza lake la mawaziri siku yoyote kuanzia jana, na
aliondoka Dodoma kwa ndege majira ya saa mbili asubuhi.
Kuwapo kwake kwa siku nyingi katika kijiji cha Chamwino akifanya kazi,
kulipongezwa na wanakijiji hao. Aidha, wanazuoni na wanasiasa
walitafsiri uwapo wake kijijini hapo kuwa ni kujichimbia asibughudhiwe
wakati akipanga baraza lake la mawaziri na mfumo wa uendeshaji mpya wa
baraza hilo.
Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Rais atateua Baraza la Mawaziri kwa
kushauriana na Waziri Mkuu na Makamu wa Rais, hivyo kuna kila dalili
wawili hao kama sio wote watatu, wameshafanya kazi hiyo.
Ofisi ya Waziri Mkuu ilithibitisha Dk Magufuli kutinga ofisini kwa
Waziri Mkuu, Majaliwa na kufanya mazungumzo ya takribani saa moja.
“Rais aliingia ofisini kwa Waziri Mkuu Majaliwa majira ya saa tisa na
kulakiwa na mwenyeji wake na baadaye walikaa kwa mazungumzo yao wawili
tu.
“Baada ya mazungumzo hayo, Rais alizungumza kwa muda mfupi sana na
makatibu Muhtasi wa Waziri Mkuu kabla ya kuondoka kuelekea Ikulu,”
ilieleza taarifa fupi ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mapema wiki hii, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisemakuwa
Rais akishakamilisha kazi hiyo ya kuteua Baraza la Mawaziri waandishi wa
habari watajulishwa ili waupashe habari umma wa Watanzania.
Akilihutubia Bunge na wakati akiwa katika mikutano yake ya kampeni za
Uchaguzi Mkuu, DkMagufuli aliahidi kuunda Baraza la Mawaziri dogo ikiwa
ni mojawapo ya njia za kudhibiti matumizi ya serikali kwa nia ya
kutafuta majawabu ya kero za wananchi kwa kasi inayostahili.
Na hilo tayari limeonekana katika hatua kadhaa ambazo amezichukua tangu
aingie Ikulu. Alianza kwa kusitisha safari za nje zisizo na umuhimu
mkubwa, sherehe za Uhuru na kuzipa mwelekeo mwingine kwa mwaka huu na
pia kusitisha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi.
Katika kipindi kifupi cha uongozi wake, maamuzi mazito kuhusu namna
anavyotaka nchi iende yamefanyika ikiwa na kuhimiza ukusanyaji wa kodi
kwa kufanya ziara ya kushtukiza Hazina na pia Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili ambako alivunja Bodi kabla ya kutumia fedha za sherehe za
uzinduzi wa Bunge (mchapalo) kiasi cha Sh milioni 225 kutumika kuboresha
hali ya Hospitaliya Taifa ya Muhimbili.
LIKE PAGE YETU HAPA CHINI
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by NDALIKE SONDA MEDIA
Post a Comment