0

UNAWEZA KUJIUNGA NASI HAPA MOJA KWA MOJA ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..



WAZIRI Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, amefanya ziara ya kushtukiza bandarini Dar es Salaam leo na kuwaita maofisa wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kikaoni kujadili changamoto kuhusu ufanisi na mapato
Katika ziara yake hiyo, ameamuru kukamatwa kwa maafisa kadhaa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na wengine kufukuzwa kazi baada ya kukuta mapungufu mengi ambayo hayakumfurahisha.

Taarifa zilizoifikia blogu hii leo Novemba 27, 2015 zinaeleza kuwa maofisa hao wametakiwa pia kusalimisha hati zao za usafiri kwa lengo la kufanikisha uchunguzi wa Jeshi la Polisi dhidi ya tuhuma zinazowakabili.
Waziri Mkuu
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea na viongozi wa TRA na TPA
Aidha, ziara hiyo imebaini kuwa ziara ya Waziri huyo mkuu ilikuwa na lengo la kuangalia jinsi TPA inavyofanyakazi kwa pamoja na TRA na kujua ni kwanini Serikali inapata taarifa ya kuwepo kwa mizigo inayotoka ndani ya Bandari hiyo kwenda nje bila kulipiwa.
"Kuna watu wapo geti namba tano ambao wanapitisha mizigo, na wapitishaji ni wale wale, anayekaa zamu leo na kesho ni huyo huyo ndiye anayefanya zoezi hili"
 
Ametishia kuwafukuza kazi walinzi wa mageti yote ambao watabainika kuhusika na ubadhilifu huo, na kwamba kama jambo hilo litafanikiwa utaandliwa mpango mwingine wa kutatua tatizo hilo haraka iwezekanavyo.
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, akisalimiana na maofisa wa TRA pamoja na wale wa TPA baada ya kufanya ziara hiyo
kwa mujibu wa chanzo chetu, hatua ya Waziri Mkuu kuagiza kukamatwa kwa maofisa hao ni pale ilipogundulika kwamba kuna makontena takribani 349 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 80 ambayo taarifa zake ndani ya Mamlaka ya Bandari zipo lakini katika mtandao wa TRA hayaonekani.
Uchunguzi huo pia utawahusu madereva wa magari waliokuwa wanatumika kutoa mizigo mbalimbali nje ya bandari hiyo, hivyo suala la kujulikana kwamba mzigo ulilipiwa fedha za ushuru ama la litajulikana.
Waliosimamishwa kazi ni pamoja na Kamishna wa Kodi, Tiagi Masamaki na Habibu Mpozya Kitengo cha Huduma kwa Wateja kutokana ubadhilifu wa fedha kwa makontena hayo.
Wengine ni Haruni Mpande -ICT, Hamisi Ali Omari na Eliachi Mrema, Mkuu wa kitengo wa ICD na pia wapo waliohamishwa kituo na kupelekwa mikoani ambao ni pamoja na Nsajigwa Mwandege, Robert Nyoni na Anangisye Mtafya.

Chanzo ni Fikira Pevu
www.ndalike.blogspot.com 

LIKE PAGE YETU HAPA CHINI

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Facebook Plugin by NDALIKE SONDA MEDIA

Post a Comment

 
Top