UNAWEZA KUJIUNGA NASI HAPA MOJA KWA MOJA ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Kundi la watu wasiao fahamika wamechoma nyumba ya mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Mwalugulu kata ya mwalugulu wilayani hapa na kisha kumwandikia barua ya kumtishia maisha yake wakimtaka ahame katka kijiji hicho.
Tukiko la kuchomwa kwa nyumba hiyo limetokea mwisho mwishon mwa wiki iliyopita na siku ya juma tatu alikuta barua hiyo ikimtaka ahame katika kijiji hicho.
Akizungumza juzi mwenyekiti huyo alisema barua hiyo Paul Masule aliikuta jirani na zizi lake ikiwa imebandikwa huku ikimtaka ahame aende mbali zaidi kwa usalama wake.
"Nyumba yangu ilichomwa ijumaa iliyopita, halafu jumatatu nilipoamuka nikamwanbiwa mtoto wangu aende kugagua mifugo alipofika aliona barua ndio akamwita ili aisome nilipoenda nikaisoma inasema kwamba nihame utemi tisa au majimbo tisa."alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha alisema huenda chazo cha tukio hilo ni kutokana na oporasheni inayoendeshwa katika kijiji hicho cha kuwabaini kwa kuwapigia kura za siri wahalifu.
Naye Kaimu afisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Masanja Mathias alisikitishwa na vitisho hivyo ambavyo viongozi wameanza kufanyiwa na aliwaomba wananchi kuwa na Ushirikiano kuwabaini wahalifu..
www.ndalike.blogspot.com
LIKE PAGE YETU HAPA CHINI
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by NDALIKE SONDA MEDIA
Post a Comment