UNAWEZA KUJIUNGA NASI HAPA MOJA KWA MOJA ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Akizungumzia juu ya tukio hilo ,kamanda wa polisi mkoani Pwani,Boniventure Mushongi, alisema
mwenyekiti huyo alifariki akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya mission ya Mchukwi baada ya shambulio hilo.
Alieleza kwamba tukio hilo limetokea desemba 5,majira ya saa mbili usiku,wakati mwenyekiti huyo akirejea nyumbani kwake akiwa na mpenzi wake Sophia Maulid(40)katika kitongoji cha Besabu kijiji cha Nyambunda kata ya Bungu.
“Ndipo walipotokea watu watatu wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki aina ya boxer isiyokuwa na namba na kuwaamuru kusimama kisha kumpiga risasi ya tumboni na mapanga ya kichwani”alisema.
Kamanda Mushongi,alieleza kuwa jeshi hilo mkoa linaendelea kufanya msako mkali kuwasaka wahusika wa tukio hilo ambapo amewaomba wananchi kuwapa ushirikiano kuwafichua wahusika ili waweze kuwachukulia hatua.
Kamanda Mushongi alisema hilo ni la nne kutokea likihusisha viongozi wa serikali za vijiji na vitongoji wilaya ya Mkuranga na Kibiti.
“Hivi karibuni mtendaji wa kijiji cha Nyambunda ,kata ya Bungu wilaya ya Kibiti ,Ally Omary Milandu (58),nae alipigwa risasi ya kisogoni na kutokea mbele ya paji la uso na watu wasiojulikana na kufa papo hapo”alisema.
Katika hatua nyinyine miili ya watu sita wakiwa wamefariki dunia ,imeokotwa huku katika eneo la mto Ruvu kata ya Makurunge,wilayani Bagamoyo mkoani hapo, huku ikiwa imeharibika vibaya .
Kamanda Mushongi alisema miili hiyo imeokotwa desemba 6 majira ya saa tano asubuhi baada ya jeshi hilo kupatiwa taarifa kutoka kwa raia wema wanaojihusisha na kilimo na uvuvi kwenye mto Ruvu .
Kamanda Mushongi alifafanua ,wasamaria wema hao waliona miili hiyo ikielea juu ya mto ikiwa imekufa ndipo walipofuatilia na kwa nyakati tofauti waliweza kubaini miili ya watu watano ambao hawakuweza kufahamika majina yao mara moja.
Hata hivyo alisema watu hao wote ni jinsia ya kiume wakikadiriwa kuwa na umri wa miaka 25-35 ikiwa imetepeta kwa kukaa kwenye maji na kuanza kuharibika vibaya.
Kadhalika tarehe 7 desemba mwili wa mtu mwingine anaekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25-30 uliokotwa na hivyo kufanya idadi ya miili ya watu waliokufa kwa maji kufikia sita.
Kamanda Mushongi alieleza ,kutokana na miili hiyo kuharibika imefanyiwa uchunguzi na daktari kuamriwa izikwe.
Alisema wanafuatilia kwasasa kujua miili hiyo ilitokea wapi hadi kufika kuokotwa mkoani Pwani kwani inaonyesha ilisafirishwa na maji umbali mrefu kwa namna maiti hizo zilivyokuwa kwenye hali mbaya.
www.ndalike@yahoo.com
LIKE PAGE YETU HAPA CHINI
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by NDALIKE SONDA MEDIA
Post a Comment