UNAWEZA KUJIUNGA NASI HAPA MOJA KWA MOJA ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
WAKAZI wa Kijiji cha Mwakata Wilayani Kahama Mkoani
Shinaynga walioathirika na mvua ya mawe iliyonyesha hivi karibuni huwenda
wakapata makazi yakudumu na kuhama katika Shule ya msingiMwakata walipokuwa
wameweka kambi kutokana
na baadhi ya makampuni ya ujenzi kuanza kutoa misaada kwa ajili ya ujenzi wa
makazi mapya.
Baadhi ya
Makampuni yalioanza kutoamsaada huo kwa wahanga haonipamoja na Kampuni ya
Mwanza huduma Limited Iliyotoa Jumla yamifuko 560 kwa ajili ya kusadia ujenzi
wa Makazi mapya kwa wahanga hao pamoja Kampuni ya Airtel Tanzania iliyotoa
Jumla ya mabati100.
Pia
Kampuni Simba Cement ya Jijini Tanga pia imetoa Msaada wa Mchele kilo 1,500,
Unga Mahindi kilo 1,500,Mafuta ya kupikia Lita 500 Sukari
kilo200,Madaftari Katoni 60, Blankets pisi 300 pamoja na box nne za Kalamu kwa
ajili ya Wanafunzi waliokumbwa na matatizo hayo ya Mvua ya mawe.
Kampuni hiyo ya Simba sementi kupitia
wakala wake aliyopo Mjini Kahama Engan Enterprises ya Mjini Kahama imehaidi
kuendelea kusadia wahanga hasa katika sekta yaujenzi ili waweze kufanikiwa
kupata makazi mapyanakuanza kuishi kama ilivyokuwa hapo awali.
Kwa upande
wake Meneja Biashara wa Kampuni ya Simba Cement Matheus Roose alisema kuwa misaada hiyo waliotoa wanaimani kuwa
itawasaidia wahanga na kuongeza kuwa waokama wadau wameguswa na tukio hilo
ambaloni la kihistoria hapa nchini.
Kwa uapnde
wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akipokea misaada hiyo alisemakuwa
kwa sasa misaada kamahiyo kwa ajili ya Ujenzi ndiyo inahitajika kwa wahanga hao
ilikurahisisha kupungua katika kambi nakusababisha Wanafunzi kukosa masomo hadi
kufikia hivi sasa.
"Wanafunzi hawa wa shule ya Msingi Mwakata
waliopo likizo kwa sasa kupisha wahanga hawa lazima waanze shule mara moja na
kwa wasamaria wema kuanza kuleta vifaa vya ujenzi kamavile mabati Saruji na
vinginevyo vitasadia kwa wahanga hawa kuanza kujenganyumba zao upya na
kupunguza msongamano katikashule hiyo”, Alisema Rufunga.
Pia
aliongeza kuwa kwa sasa ni lazima kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaanza masoma
mara moja na tutaanza mikakati yakuihamisha kambi hii ndani ya sikumbili
nikibali tulichopewa naWizara ni cha kuwahifadhi kwa siku hizo na si vinginevyo.
LIKE PAGE YETU HAPA CHINI
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by NDALIKE SONDA MEDIA
Post a Comment