UNAWEZA KUJIUNGA NASI HAPA MOJA KWA MOJA ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Mbunge wa jimbo la Msalala
wilayani Kahama mkoani Shinyanga Ezekiel Maige ametoa mashine ya kudurufu
karatasi kwa shule ya sekondari Mwalimu Nyerere iliyopo Kata ya Segese ili kusaidia
uchapishaji wa mitihani wa wanafunzi kufanyika shuleni hapo.
Akizungumza wakati wa
kukabidhi mashine hiyo mbele ya viongozi
wa Kata hiyo, wazazi, walimu,na wanafunzi Maige alisema mashine hiyo ni ahadi aliyoahidi wakati wa
mahafari ya kidato cha nne mwaka jana
shuleni hapo huku gharama ya kifaa hicho kikiwa ni shilingi milioni 5.
Alisema aliamua kuahidi na kutoa msaada huo kutokana
na kuwepo kwa changamoto kubwa ya uchapishaji wa mitihani kwa licha ya kwamba
shule hiyo ina umeme unaotumia nishati ya Juan a kwamba walimu na wanafunzi
waitunze mashine hiyo ili iweze kudumu na kuwasaidia katika kuarahisisha kazi
zao.
Katika hatua nyingine Maige
aliwapongeza wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule hiyo kwa jitihada
wanazozionesha katika kuboresha miundombinu ya shule hiyo hali ambayo
imesabaisha kuendelea kuinua kiwango cha elimu katika shule hiyo ambapo katika
miaka ya hivi karibuni ni miongoni mwa
shule zinazofanya vizuri kwa upande wa taalum mkoani Shinyanga.
Kwa upande wake mkuu wa
shule hiyo Peter Kweba alisema mashine
hiyo itasaidia kupunguza makali ya matumizi ya fedha kwa shule hiyo kwani awali walikuwa wakitumia zaidi ya
shilingi milioni 12 kwa mwaka ambapo kila mtihani walikuwa wakitumia zadi ya
shilingi milioni 3 kudurufu mitihani.
Aidha baadhi ya wazazi na
wanafunzi walimpongeza Mbunge Maige kwa kuzidi kujali wananchi wa jimbo la Msalala katika sekta zote ambapo
wakizungumzia msaada huo walisema
imepunguza usumbufu wa michango iliyokuwa ikitolewa kwa ajili ya
uchapishaji wa mitihani.
LIKE PAGE YETU HAPA CHINI
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by NDALIKE SONDA MEDIA
Post a Comment