UNAWEZA KUJIUNGA NASI HAPA MOJA KWA MOJA ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Mwanasheria
mkuu wa chama cha upinzani nchini CHADEMA, Tundu Lissu leo ametangaza
kuvuliwa uanachama kwa mbunge wa Kigoma Kasikani Zitto Kabwe baada ya
Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam kutupilia mbali
pingamizi la mbunge huyo la kuzuia asijadiliwe.
"Kwa
mujibu wa katiba ya chama cha CHADEMA, mwanachama yoyote anapofungua
kesi mahakamani dhidi ya chama chake, endapo atashindwa katika kesi hiyo
atakuwa amejiondoa uanachama wake, kwahiyo natangaza rasmi rasmi Zitto
Kabwe sio mwanachama tena wa Chadema.
Kwa
upande wake Zitto Kabwe amesema hawakuwa na wito wa mahakamani leo na
Jaji wa kesi kahamishiwa Tabora na hawana taarifa ya Jaji Mpya, pia
kaongeza kuwa Mwanasheria anafuatilia na atatoa statement.
Licha
ya kutupilia mbali kesi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe,
Mahakama kuu imemtaka kulipa gharama zote za kesi toka ilivyoanza.
Mwaka
jana Zitto Kabwe aliweka pingamizi mahakamni kuzuia kikao cha Kamati
Kuu kumjadili na hoja yake ilikuwa ni kupinga kuitisha kamati kuu kabla
shauri lake kusikilizwa na Baraza Kuu.
LIKE PAGE YETU HAPA CHINI
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by NDALIKE SONDA MEDIA
Post a Comment