UNAWEZA KUJIUNGA NASI HAPA MOJA KWA MOJA ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Kukamilika kwa mradi wa
umeme vijijini katika Kata ya Bulige halmashauri ya Msalala wilayani Kahama
mkoani Shinyanga kutasaidia kuongeza mapato ya ndani yanayokuswanwa na
halmashauri hiyo kutokana na kwamba wamekusudia kuweka soko la kimataifa la
mchele katika kata hiyo.
Akizungumza na wanachi wa
Kijiji cha Segese kata ya Segese, Mbunge wa jimbo la Msalala Ezekiel Maige
alisema tayari katika kijiji cha Bulige wametenga eneo kwa ajili ya soko hilo
ambalo litasaidia mpunga unaozalishwa katika halmashauri hiyo kukobolewa na
kuuzwa katika soko hilo na hivyo kuiingizia
mapato ya ndani halmashauri hiyo.
Maige alisema hali hiyo
itasaidia kukusaya ushuri unaotokana na mapato hayo zaidi ya shilingi Milioni
500, kila mwaka hali ambayo itasaidia kuinua uchumi wa wananchi wa halmashauri
hiyo.
Alisema mbali na soko hilo
pia amebainisha mapato mengine ya ndani ambayo yataisaidia halmashauri
kujiendesha ni pamoja na kupata
ushuru kutoka katika kampuni ya
uchimbaji madini ya ACACIA kupitia mgodi wa Bulyanhulu pamoja na makampuni
yanayofanya kazi ndani ya mgodi huo ambayo nayo waliingia mkataba wa kulipa
ushuru kwa halmashauri.
Maige alisema hali hiyo
itasaidia pia kuwepo kwa mkakati wa
kufuta michango mbalimbali kwa wananchi kwani halmashauri itakuwa ikijiendesha
yenyewe bila kutegemea michango ya wananchi.
LIKE PAGE YETU HAPA CHINI
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by NDALIKE SONDA MEDIA
Post a Comment