UNAWEZA KUJIUNGA NASI HAPA MOJA KWA MOJA ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Chama cha Demokrasia na
maendeleo CHADEMA kimetoa msaada wa Mabati 850 sawa na bando 50 ambayo ni ahadi
iliyotolea na mwenmyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe kusaidia
waathirika wa mvua yam awe katika kata ya Mwakata wilayani Kahama.
Akizungumza wakati wa
kukabidhi msaada huo, Katibu wa chadema, Dr. Wilbroard Slaa alisema msaada huo
unathamani wa shilingi Milioni 12, ambapo shilingi milioni 10 ilitolewa na
chama hicho kupitia ruzuku inayotolea na serikali kwa chama hicho huku shilingi
milioni mbili ilipatikana katika mikutano iliyofanywa na chama hicho mjini
Kahama.
Alisema waliambua kununua
mabati hayo kutokana na kamati ya mkoa inayoratibu mafa hayo ikiongozwa an mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Ali Rufunga kupendekeza vinunuliwa vifaa vya ujenzi kutokana na kwamba chakula kimekuwa kikitolewa
na wadau wengi.
Dr. Slaa aliwataka viongozi
kuhakikisha wanasimamia vema ujenzi wa nyumba za kuduma za makazi ya wananchi
wa kata ya Mwakata kama ilivyopendekezwa
na rais Jakaya Kikwete alipotembelea eneo hilo kwani mara nyingi serikali imekuwa ikishindwa
kutekeleza kwa wakati majanga ya aina hiyo.
“Niombe tu viongozi wa
Shinyanga simamieni waathirika hawa wajengewe nyumba kwa muda mwafaka, unajua
Watanzania wengi tanawakatisha tama kutokana na kushindwa kutimiza ahadi
zinazotolewa, kule Klosa hadi leo bado watu wananishi kwenye mahema, tangu mimi
nikiwa mwenyekiti wa Kamati ya kudumu katika Bunge, Naomba sana Shinyanga Muwe
Mfano.”alisema Slaa.
Katika hatua nyingine
misaada imeendelea kutolewa kwa
waathirika ambapo kampuni ya simu za Nchini, TTCL lilitoa msaada wa chakula na
vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 3.
Akizungumza Meneja wa TTCL
mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru alisema
TTCL imeungana na Watanzania wengeine walioguswa na Maafa hayo huku
akiyataka mashirika na watu mbalimbali kuendelea kujitokeza kuwasaidia
wananchi walioathirika.
picha zote na malunde blogu
www.ndalike.blogspot.com
LIKE PAGE YETU HAPA CHINI
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by NDALIKE SONDA MEDIA
Post a Comment