0

UNAWEZA KUJIUNGA NASI HAPA MOJA KWA MOJA ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..

Mchezo Maalumu wa kuchangia wathirika wa mvua ya mawe katika kata ya Mwakata kati ya Ambasador Sc, na Kagongwa united umeahilishwa  kutokana na mkurugenzi wa  Klabu ya Kagongwa united  Dogo Mshashi Kufiwa na Baba yake Mzazi  usiku wa kuamkia leo, "jumamosi"


Mchezo huo ambao ulikuwa uchezwe kesho jumapili katika uwanja wa shule ya Msingi Kagongwa umeahirisha na sasa utapangwa tena wiki ijayo  ambapo utachezwa katka uwanja huo na fedha zitakazopatikana zitapelekwa kwa waathirika wa mvua ya mawe kata ya Mwakata.

Akizungumza na Blogu hii Naohadha wa Kagongwa united Gabriel Lucas alisema  timu hiyo imepokea kwa masikitiko makubwa  msiba huo ambapo mazishi yatafanyika kesho katika  makaburi ya waasilamu Kagongwa  na hivyo mamshabiki kuendelea kuwa  na subira juu ya mchezo huo.

Kwa uapende wake Msemaji wa Ambasador Fc Ndalike Sonda alisema baada ya kutokea kwa msiba huo, wanasubiri raitba ya mashindano ya ligi daraja la kwanza hatua ya sita bora ili kupanga mchezo huo kufanyika.
"Kwa kweli kwanza tumepokea kwa masikitiko makubvwa msiba huu, ila tunaomba tu mashabiki muendelee kusubiri bila shaka ratiba ya mkoa itakapotoka tutawafahamisha  ili mjie kuchangia michango ambayo tutawapelekea wenzetu wa Mwakata" alisema Kocha Mkoangwe
www.ndalike.blogspot.com

LIKE PAGE YETU HAPA CHINI

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Facebook Plugin by NDALIKE SONDA MEDIA

Post a Comment

 
Top