UNAWEZA KUJIUNGA NASI HAPA MOJA KWA MOJA ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Mwanasoka
raia wa Tanzania anayechezea TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC) Mmbwana Ally Samatta amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa
Afrika anachezea ndani ya bara la Afrika, wakati tuzo ya mwanasoka bora
barani Afrika ikienda kwa Pierre-Emerick raia wa Gabon anayesakata
kabumbumbu katika klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Tuzo
hizo za kila mwaka zinazotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika
almaarufu kama CAF zimetolewa usiku kuamkia leo mjini Abuja nchini
Nigeria.
Kwa
upande wa timu ya wanawake ya mwaka tuzo imekwenda kwa timu ya
Cameroon. Timu bora kwa wanaume kwa mwaka uliopita ni kutoka Ivory
Coast.
Kocha
bora wa mwaka ni – Herve Renard, kutoka Cote d’Ivore ambayo inashinda
kwa mwaka wa pili mfululizo wakati Klabu bora ya soka barani Afrika ni –
TP Mezembe, kutoka DR Congo ambapo mwanasoka bora wa kike Afrika ni
Gaelle Enganamouit kutoka Cameroon na Mwamuzi bora wa mwaka ni – Bakary
Gassama kutoka nchini Gambia.
Tuzo
hizo zilipambwa na shamra shamra za kila aina kutoka kwa wasanii
maarufu pamoja na wanenguaji walitumbuiza akiwemo mwanamuziki nguli
kutoka nchini Mali, Salif Keita pamoja na mwanamuziki kutoka Nigeria
Omowumi.
LIKE PAGE YETU HAPA CHINI
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by NDALIKE SONDA MEDIA
Post a Comment