UNAWEZA KUJIUNGA NASI HAPA MOJA KWA MOJA ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Na Ndalike Sonda, Kahama.
12/11/2016.
Mkuu
wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu amewaagiza
maafisa afya na mazingira katika
Kila kata wilayani humo kuhakikisha wanawafikisha mahakamani wananchi wote
wanaokamatwa kwa kosa la kukaidi agizo la usafi wa mazingira katika maeneo yao.
Akizungumza na Waandishi wa
habari, Nkurlu amewataka maafisa hao watumie sheria ya afya ya jamii namba 1 ya mwaka 2009.
Nkurlu amewataka wananchi
kujitokeza kwa wingi kesho ili
kufanya usafi katika maeneo yao
kama agizo la serikali ya wilaya hiyo linavyoelekeza.
Wakati huo huo Nkurlu
amewaonya wamiliki wa Migahawa, nyumba za kulala wageni na makampuni ambao
wanatiririsha maji machafu kwamba serikali imekusudia kuwachukulia hatua za
kisehria.
LIKE PAGE YETU HAPA CHINI
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Facebook Plugin by NDALIKE SONDA MEDIA
Post a Comment